Post: JUMIKITA YAPEWA MAFUNZO MAALUM YA KANUNI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

JUMIKITA YAPEWA MAFUNZO MAALUM YA KANUNI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dkt. Grace Magembe, amesema wizara hiyo imeandaa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa lengo la kuendana na usawa na umuhimu wa kutumia mitandao kwa kuwafikia wananchi. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Katika mkutano huo, TAMISEMI ilikutana na Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), chini ya uongozi wa Mwenyekiti Shabani Matwebe, kwenye ofisi za TARURA jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mafunzo maalum ya kanuni za uchaguzi.

Dkt. Magembe alisisitiza umuhimu wa waandishi kuzingatia weledi, kutoa taarifa za kweli na zenye kuaminika, zinazochangia umoja wa kitaifa na kuimarisha upendo na amani. Aliongeza kuwa taarifa zinapaswa kuzingatia muda na kutokuchochea mgawanyiko au taharuki. Aidha, aliwataka waandishi kuhakikisha taarifa wanazotoa hazina upendeleo, bali zinazingatia haki kwa vyama vyote.

Social Media
Facebook
Twitter
WhatsApp
LinkedIn
Scroll to Top