Post: Viongozi wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni Zanzibar Watembelea Ofisi za JUMIKITA Dar es Salaam

Viongozi wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni Zanzibar Watembelea Ofisi za JUMIKITA Dar es Salaam

Viongozi wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni Zanzibar (ZONA) leo wametembelea ofisi za Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni Tanzania (JUMIKITA) zilizopo jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo ya siku moja, Mwenyekiti wa ZONA, Ali Seif, akiwa ameongozana na wajumbe Rashid Ali na Khamis Hulela, walikutana na Mwenyekiti wa JUMIKITA, Shabani Matwebe, kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na jumuiya hiyo.

Mazungumzo yao yalilenga kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano kati ya jumuiya hizo mbili kwa faida ya wanahabari wa mitandaoni nchini.

Social Media
Facebook
Twitter
WhatsApp
LinkedIn
Scroll to Top