SISI
Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) ni shirika lililoanzishwa mwaka 2021 na lengo la kuwainua wanahabari nchini. JUMIKITA imejitolea kuwaunganisha na kuwasaidia wanahabari wa mitandao ya kijamii ili kuboresha uwezo wao wa kitaaluma, kuongeza ufahamu wa umma na kukuza uhuru wa kujieleza.