Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Jumuiya ya Waandishi wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) kwa kufanya vyema katika kutoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii.
Pongezi hizo zilitolewa leo kwenye kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari linaloendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari linaloendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Jumuiya ya Waandishi wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA) iliwakilishwa na Mwenyekiti, Shaban Matwebe, Makamu Mwenyekiti Humphrey Shao, Yasin Ng’itu (Mjumbe) na Dr. Bravious Kahyoza (Mshauri wa Utendaji). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza JUMIKITA kwa kufanya vyema katika kutoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii.