Post: TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

KONGAMANO LA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO YA KIJAMII LINALOANDALIWA NA JUMIKITA KWA KUSHIRIKIANA NA TAHLISO

JUMIKITA (Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania) kwa kushirikiana na TAHLISO
(Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania) inaandaa Kongamano la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii nchini litakalofanyika tarehe 20/5/2024 kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.


JUMIKITA inapenda kuutaarifu umma kuwa, Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili undishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo. Pamoja na dhima hiyo kuu, Kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ikia ni pamoja na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.


Aidha, Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500, litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.


Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kutoa mchango wa kiundeshaji kwa wadau kupitia JUMIKITA na mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa taarifa (information economy)


JUMIKITA inawakaribisha wote kwenye Kongamano hili muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.

Mawasiliano
Mwenyekiti JUMKITA~ Shaaban Matwebe~0717073534


Sekretarieti~
Dickson Frank Mushi~0686379370

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Posts
Social Media
Facebook
Twitter
WhatsApp
LinkedIn
Scroll to Top